Swahili

 

Mapendekezo Kwa Bodi Ya Kudhibiti Ranch

Kubuniwa bodi ya kutathmini shughli zinazoendeshwa Ranch zilizopo kaunti ya Taita Taveta kumetajwa kama suluhu la vita dhidi ya utumizi hovyo wa raslimali zilizopo kaunti hiyo sawia na kudhibiti ufugaji haramu.

Wakiongea walipomtembelea gavana Samboja afisini mwake mjini Voi, viongozi wa utawala na  wa kisiasa wakiongozwa na aliyekuwa mbunge wa Voi Basil Mwakiringo, mwakilishi wodi wa kasighau Ibrahim Juma na chifu wake Johane Mwazaule, viongozi hao wamemtaka gavana kubuni kwa haraka bodi hiyo hatua itakayo fanikisha kupatikana wawekezaji kwa urahisi.

Mwakiringo amemtaka gavana Samboja kuikabidhi bodi hiyo mamlaka ya kuwekea vikwazo chama cha kusmamia ranch kaunti hiyo TAITA TAVETA RANCHERS ASSOCIATION kuijulisha

serekali ya kaunti mikakati yote wanayoendesha haswa ya miradi. Read more......